Tmu ya Newcastle United chini ya mwalimu Eddie Howe inaendelea kuisuka timu yao kadri siku zinavyoenda.

Baada ya kupata sare dhidi ya Manchester City jumapili iliopita na kuwapa mechi mgumu sana Mabingwa hao wa ligi kuu Uingereza wamefanikiwa kumnasa mshambuliaji raia wa Brazil aliekua anaitumikia Watford Joao Pedro.

newcastle, Newcastle United Yamnasa Joao Pedro., Meridianbet

Newcastle ambao wamenunuliwa na tajiri kutoka falme za kiarabu wamekua wakifanya sajili zinazolenga kuiinua klabu hiyo kwenda kua klabu shindani kwenye ligi kuu ya Uingereza siku za mbeleni.

Na mwalimu aliopewa kazi ya kuitengeneza hiyo Eddie Howe anaonekana kuifanya kazi hiyo toka alipopewa timu hiyo mwishoni mwa msimu uliomalizika. Lengo la tajiri wa klabu hiyo ni kuifanya klabu hiyo kua miongoni mwa timu tishio ndani uingreza kwasababu suala la pesa kwa upande wake sio tatizo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa