Kocha wa Manchester United Eric Ten Hag ameonesha kufurahishwa na kiwango kilichoonshwa na vijana wake katika mchezo dhidi ya mahasimu wao wakubwa klabu ya Liverpool.
Mchezo huo ambao ulipigwa katika dimba la Old Trafford ambapo ilishuhudiwa United wakichomoza na ushindi wa goal mbili kwa moja magoli ya Jadon Sancho na Marcus Rashford huku goli pekee la Liverpool likifungwa na Mohamed Salah.
Eric Ten Hag wakati anafanya mahojiano baada ya mchezo huo alionesha kufurahishwa na kiwango cha wachezaji wake huku akigusia kwenye suala la kujitoa kwajili ya timu ameeleza wachezaji wake walijitoa na kupambania timu.
Pia amegusia namna timu inaweza kufanikiwa kwasababu wanaweza kucheza vizuri na mfano mzuri ni mchezo wa jana. Wakati huohuo mwalimu huyo amewakumbusha wachezaji wake kua wanahiaji kuonesha hali ya upambanaji kwenye michezo ijayo isiishie mchezo wa jana kwani ligi kuu ya Uingereza kila mchezo ni mgumu kushinda alisema kocha huyo.
Eric ambae ndo ameshinda mchezo wake wa kwanza kama kocha wa klabu hiyo pia aliwasifu wachezaji wake wawili Bruno Fernandes na Raphael Varane kwa kuonesha hali ya uongozi uwanjani na kusisitiza sio tu hao wawili anahitaji viongozi wengine zaidi kwenye kikosi chake.