Kiungo alieitumikia klabu ya Real Madrid kwa mafanikio makubwa na kudumu hapo kwa takribani miaka tisa Carlos Casemiro ameagwa rasmi jana jumatatu.
Katika ghafla hiyo ya kumuaga nyota huyo wa ambae anaelekea klabu ya Manchester United ilihudhuriwa na wachezaji tofauti wa klabu hiyo pamoja na kocha wa klabu hiyo Carlo Ancelotti, Pia waliowahi kua magwji wa klabu hiyo kama Raul Gonzalez Blanco.
Ghafla hiyo ambayo iliongozwa na rais wa klabu hiyo Florentino Perez ambaye alimtakia kila la kheir mchezaji huyo kuelekea klabu yake mpya.
Casemiro mwenyewe alieleza mambo mengi huku akiwashukuru mashabiki wa klabu hiyo kwa ushirikiano waliomuonesha toka anafika mpaka anaondoka na kuwaahidi atawabeba kwenye moyo waake siku zote na atabaki kua shabiki wa Real Madrid.
Pia hakusita kuwashukuru wachezaji wenzake walioshirikiana kuleta mafanikio ya klabu kwa kipindi chote alichokua hapo.
Casemiro pia alidokeza kuhusu anayoelekea na kueleza anakwenda kwenye moja ya klabu kubwa duniani na ni changamoto nzuri kwake pia ameahidi kujitoa kwa klabu hiyo kwajili ya mashabiki na timu kwa ujumla na ndoto yake kubwa ni kubeba taji la ligi kuu ya uingereza.