Serengeti Girls, Yatoboa Robo Fainali ya World Cup U17 2022

Serengeti Girls Timu ya Taifa wa wanawake umri chini ya miaka 17
(U-17) katika Fainali za kombe la Dunia la FIFA 2022 zinazoendelea kufanyika nchini India.

Leo 18 Oct 2022 ni siku ya Hostoria kwa soka la Tanzania kwani walichokifanya mabinti zetu uwanjani ni kitu kukubwa sana na kuweka historia ya kuingia katika hatua ya Robo fainali ya mashindano haya ya Fainali za kombe la dunia yaliyokuwa na Mataifa 16.

Serengeti Girls
Serengeti Girls

Tarehe 12 Oct
-Japan 4-0 Tanzania

Ilikuwa mechi nzuri kwa Serengeti Girls kwa kuwa ndio iliyotumika kurekebisha makosa kutokana na kiwango na kasi waliyokuwa nayo wachezaji wa Japan ambao wenginwao ni wafupi kwa kimo lakini kasi na footwork ilithibitika kuwa ni ya kiwango cha juu, lakini pia upungufu wa wachezaji kwa zaidi ya Dak 70 ulionekana kuwa na madhara makubwa.

Serengeti Girls

Tarehe15 Oct 2022
France 1- 2 Tanzania

Tactical Disclipline. Nidhamu ya wachezaji kufuata maelekezo ya benchi la ufundi ilikuwa ni kiwango cha juu.
Mafunzo ya watoto wenye umri chini ya miaka 17(U -17) hujikita kwenye performance base lakini Bench la ufundi kufanikiwa kutekeleza Result oriented style of play kwa vijana ni kitu kikubwa sana(Hobgera bench la ufundi). Experience has no substitute (kitendo cha kuweka kambi nchini Uingereza na kucheza mechi za kirafiki za kimataifa kabla ya kuja kwenye mashindano haya kina mchango mkubwa sana physically na mentally.

Tarehe 18 Oct 2022
Tanzanianl 1 -,1 Canada
Ilikuwa ni mechi nzuri ambayo Serengeti girls iliingia na aina ya uchezaji wa kutaka kufunga goli mapema ili kulinda ushindi huo. Bahati mbaya Canada walianza kupata goli kwa njia ya Penalty lakini Serengeti girls walionekana kuwa na commitment ya kiwango cha juu na kufanikiwa kurejesha hilo kwa shuti la umbali wa zaidi ya mita 20.


Unaweza kua kutazama video za uchambuzi na matukio ya kisoka kwa kugusa video hii

Acha ujumbe