Kiungo anayemaliza muda wake kunako Manchester United, Nemanja Matic amefikia makubaliano ya kuungana na Jose Mourinho huko AS Roma 🇮🇹 kwa mkataba mpaka Juni 2023 ambao upo ukingoni kusainiwa.
Matic (33) raia wa Serbia yupo kwenye mipango ya vipimo vya afya ambayo kufanyika Julai.
Je wajua? Jose Mourinho amemvuta Matic kwa nyakati mbili tofauti kabla ya uhamisho huu wa Roma.
Mnamo 2014, Mourinho akiwa kocha wa Chelsea alimsajili Matic kutoka Benfica.
Mnamo 2017 Jose Mourinho akiwa kocha wa Manchester United alimsajili tena Matic akimpeleka kunako Old Trafford.
Sasa akiwa kocha wa AS Roma 🇮🇹 Mourinho anaelekea kurudia yale yale huku Mreno huyo akinukuliwa kusema “Matic ni mchezaji wa Jose Mourinho”
SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!