Imeandikwa na Jemedari Said
HATUA na kila hatua duah..! Kama unajua namna Simba na Yanga zilivyohangaika na mikataba ya kulaliwa laliwa, ukiona hivi unawapongeza.

Kila upande umepata kutokana na thamani yake sokoni kwa sasa. Simba SC sio siri soko lake KIMATAIFA ni zaidi Klabu yoyote nchini.

Yanga SC kwakile ilichofanya msimu jana wanastahili walichpata pia, kwenye soko la NDANI wao ni baada ya Simba SC.

simba na yanga
simba na yanga

Matokeo ya msimu mmoja hayawezi kuwafanya kuwa juu ya Mnyama ila wanakwenda vizuri, wanapaswa kutetea Makombe yao lakini pia wafanye vyema kimataifa.

Hakuna ubishi kwamba zile robo fainali 3 mashindano ya Afrika na ubingwa mara 4 mfululizo Ligi Kuu pamoja na FA CUP 2 ndiyo umeweka tofauti na Klabu nyingine sokoni ndani na nje kwa Simba SC na kuleta 26.1B

NB: Kazi nzuri ya Baba, huleta Chakula kizuri mezani. Mnyama kafanya kazi nzuri misimu 4 wacha wapate dili nene.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa