Shirikisho la soka Tanzania (TFF) limewaasa wadau mbalimbali wa soka hususani vyama vya soka kuhakikisha vinawekeza katika soka la vijana kama sehemu ya kuendana na kasi ya ukuaji wa soka Tanzania.

Hayo yalizungumzwa na Makamu wa Rais wa TFF, Athumani Nyamlani jana Jumapili alipohudhuria mkutano mkuu wa mwaka wa Chama cha soka Wilaya ya Ubungo (UFA), uliofanyika kwenye Uwanja wa Kinesi jijini Dar es Salaam.

Soka

Mkutano huo wa kikatiba uliodhaminiwa na Kampuni ya ulinzi ya K4S Security, ulikuwa na Ajenda mbalimbali ikiwemo kufanya tathimini ya mipango ya Chama hicho katika kukuza na kuendeleza mchezo wa soka.

Nyamlani alisema: “Ni muda sasa kwa vyama vya michezo kuhakikisha vinasimamia misingi ya utawala bora kama ambavyo imefanywa na UFA kwa kuhakikisha kunakuwa na mkutano mkuu wa mwaka, ambapo huko pia ni lazima kuhakikisha tunajadili uwekezaji wa soka kwa vijana kwa ajili ya kesho ya mpira wetu.”

Naye Mwenyekiti wa UFA, Benjamin Mwakasonda alisema: “Tunashukuru kujumuika na Makamu wa rais Nyamlani na tunaahidi kufanyia kazi maagizo yake.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa