Jemedari Said Kazumari amekua ni moja ya watu wanaozungumzia kwa ukaribu sakata la manara na TFF kwa siku za karibuni, Leo kupitia kurasa wake wa Instagram ameandika andiko lefu kuhusu haji kuomba radhi kwa waziri juu ya kauli aliyo itoa siku chache zilizopita

Kwenye andiko hilo Jemedari ameandika “Kumsaidia Haji ni kumuambia UKWELI pale anapokosea tu, wanaomzunguka HAWAMPENDI kwakuwa hawawezi kumuambia ukweli mchungu ambao ni tiba kwa tabia zake.”

Jemedari Saidi
Jemedari Saidi

“Tunaoonekana hatumpendi ndio kiuhalisia TUNAMPENDA ila kwakuwa anazungukwa na WAHUNI ambao wanamuelekeza shimoni na yeye kajivika upofu ndiyo maana ndani ya siku 3 anaomba msamaha mara 2.”

Ukimuambia ukweli wewe ni adui na WAPAMBE watakuandama sana kwa maneno, lakini leo masikini ya Mungu anahangaika pekeyake na misamaha isiyoisha.

Kwa kuongezea Jemedari saidi amesema Haji HACHUKIWI ingawa yeye mwenyewe hajipendi na wanaomzunguka hawajahi kumpenda.

Wanashangilia anguko lake kwa kumvika Ufalme hewa na yeye anajiona mfalme kweli kumbe anajiingiza kwenye lindi la matatizo.

Tunaomuambia ukweli ni vile tunaochukizwa na tabia zake ambazo sio za kiuanamichezo anazozionyesha kila uchao kwa watu tofauti tofauti.

Jemedari Said

Nakukumbusha tu kumuomba msamaha Waziri na ukakiri kukosea hadharani ni vyema sana. Lakini pia unadhihirisha kwamba ulipomkosea Waziri ulifanya kosa la KIMAADILI.

Kosa la kimaadili linaweza kuishi hata miaka 10 likafufuliwa na ukashitakiwa nalo na ukaadhibiwa. Wanaokuchukia hawawezi kukuambia hivi. Sisi tunaokupenda pekee ndo tunakupa ukumbusho huu jadidi.


 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa