Carney Chukwuemeka amesaini kandarasi ya miaka sita ya kuwepo darajani. Kinda huyo mwenye miaka 18 alikuwepo kwenye kikosi kilichoshinda ubingwa wa Ulaya chini ya miaka 19 cha uingereza dhidi ya Israel huku yeye akiwa moja wa wachezaji waliofunga goli kwenye mchezo huo.
Carney mkataba wake na klabu ya Aston Villa ulikuwa unafikia tamati majira haya ya kiangazi na klabu ilipohitaji kumuongezea mkataba ili aweze kusalia kwenye kikosi cha Steven Gerrard aligoma na kuomba kuondoka.
“Imekuwa ni ngumu lakini sikuweza kuitoa chelsea kwenye akili yangu kwa siku kadhaa ila nina furaha na kuweza kumaliza hili.
“Nina furaha na nina shauku ya ya kujumuika na timu uwanjani, na kukutana na wachezaji wote na kuajaribu kushinda michezo na vikombe nikiwa na Chelsea.” Alisema Carney Chukwuemeka