Mchezaji walimataifa wa Brazili anayekipiga kwenye klabu ya Manchester United Alex Telles leo amekamilisha uhamisho wke wa mkopo kutoka klabu hiyo kwenda Sevilla kwa mkopo wa muda mrefu.

Mchezaji huyo mwenye miaka 29, alijiunga na Manchester United akitokea FC Porto mwaka 2020 na amefanikiwa kuichezea klabu hiyo michezo 50 kwenye mashandano yote.

Alex Telles, Alex Telles Atimkia Sevilla, Meridianbet

Alex Telles muda mwingi amekuwa akicheza beki namba tatu, baada ya mchezaji wa kimataifa wa Uingereza kuumia Luke Shaw. Kuwasiri kwa Tyrell Malacia kunamfanya akose namba kwenye klabu hiyo.

Sevilla wamekubali kugharamia mshahara wake wote na kwenye mkataba ambao amesaini Telles hakuna kipengere cha kumsajiri mchezaji huyo moja kwa moja kwenye klabu hiyo.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa