Marekani imeingia kwenye kinyanganyiro cha kuandaa mashindano ya FIFA Club World Cup 2023 baada ya kutofikiana makubaliano na nchi ambazo walipawe nafasi ya kuandaa mashindano hayo ambayo ni Abu Dhabi na China.

FIFA bado hawajathibitisha ikiwa mashindano yataendelea kama yalivyopangwa, huku mashindano hayo yakitarajiwa kufanyika ndani ya mwezi  February, ambapo ndio tamaduni ya msahindano hayo hufanyika huku yakijumusiha bingwa wa kila bara.

Marekani, Marekani Kuandaa Mashindano ya FIFA Club World Cup 2023, Meridianbet

Baada ya makubaliano kushindwa afikiana na Abu Dhabi na China, Marekani ndio taifa linalopewa kipaumbele zaidi kwa sasa, sababu ya kuandaa mashindano ya kombe la dunia 2026, wakishirikiana na Canada na Mexico.

Rais wa FIFA Gianni Infantino alisema anatumaini mashindano yatapiga hatua na kuwa ya kidunia kweli baada ya kuwa yatakuwa yanachezwa sehemu tofauti tofauti sio kama awali ambapo yalikuwa yanachezwa nchini Japan pekee.

Klabu zinazotarajiwa kushiriki mashindano ya FIFA Club World Cup 2023 ni Real Madrid kama bingwa wa ulaya na mshindi wa Copa Libertadores kutoka amerika ya kusini ambapo mshindi kati Flamengo na Atletico Paranaense ndiye atakayewakilisha bara hilo.

Huku Afrika ikiwakilishwa na Wydad Casablanca, amerika ya kaskazini ikiwakilishwa na Seattle Sounders wakati bingwa wa Asia mpaka sasa bado hajapatikana.

Real Madrid ndio timu pekee inayongoza kushinda ubingwa huo mara nyingi zaidi  kwenye historia huku akiwa na amebeba mataji manne huku taji lake la mwisho akichukua mwaka 2018.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa