Wydad Casablanca pamoja na klabu ya Rs Berkane watafungua michuano ya Afrika rasmi siku ya jumamosi ya tarehe 10 mwezi wa tisa kwenye Caf super cup.

Timu hizi kutoka nchini Morocco zinapata fursa ya kufungua michuano hiyo ya Caf baada ya kufanya vizuri kwenye michuano ya Afrika msimu uliomalizika na kuonekana kama vilabu kutoka nchini Morocco vilitawala michuano hiyo kwa mwaka 2022.

wydad casablancaWydad Casablanca ambao ndio mabingwa wa ligi ya mabingwa Afrika baada ya kuwafunga mabingwa wa muda wote wa michuano hiyo klabu ya National Al Ahly ya nchini Misri katika mchezo uliopigwa nchini Morocco pia Rs Berkane wanacheza Caf Super cup baada ya kushinda mchezo wa fainali ya shirikisho dhidi ya klabu ya Orlando Pirates ya nchini Afrika ya kusini hivo mchezo huo kuwakutanisha vigogo hao kutoka nchini Morocco.

Mchezo wa ufunguzi wa michuano ya Caf maarufu kama Caf super cup huwakutanisha mabingwa wa vikombe viwili vinavyosimamiwa na shirikisho hilo kwa maana ya ligi ya mabingwa Afrika pamoja na kombe la shirikisho Afrika.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa