Marco Rose kocha mpya wa klabu ya Rb Leipzig ambaye ametambulishwa wiki atakumbana na mtihanin mzito kwani michezo mwili ya kwanza ya ligi kuu nchini Ujerumani maarufu kama Bundesliga anakwenda kukutana na waajiri wake wa zamani vilabu vya Borussia Dortmund na Borussia Monchengladbach.

Rose alizungumza wakati atambulishwa “sote tunacheza ligi moja kwa hivyo tutakabiliana na kila timu kwa wakati fulani”  “akaendelea kwa kusema kwa hakika ni maalumu na ya kusisimua, lakini nina kazi nyingi za kufanya hapa hivo upangaji wa ratiba sio muhimu sana tutaichukua kadri itakavyokuja”.

marco roseMrithi huyo wa Domenico ana kibarua cha kufanya cha kuirudisha timu hiyo kwenye mstari baada ya kuanza vibaya ligi hiyo na timu ya zamani Borussia tayari wamewaacha Leipzig kwa alama saba.

Leipzig wakikusanya alama tano pekee katika mechi tano walizocheza msimu huu inaonesha Marco Rose ana kazi ya kufanya ili kuisimamisha timu hiyo na kurudi kua timu ya kutisha kama hapo awali.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa