Brendan Rodgers Achanganyikiwa

Kocha mkuu wa Leicester City Brendan Rodgers amechanganyikiwa na yupo katika wakati mgumu sana baada ya timu yake kuendelea kufanya vibaya kwenye ligi kuu msimu huu toka Epl iliporejea.

Brendan Rodgers Achanganyikiwa

Brendan amesema hayo jana kuwa waanapitia wakati mgumu baada ya timu yake kupoteza mchezo wa jana wakiwa nyumbani dhidi ya Manchester United huku kikiwa ni kipigo cha nne amekipokea baada ya kucheza mechi 5 huku akiwa ameambulia sare moja tuu mpaka sasa.

Kocha huyo amesema kuwa ni wazi kuwaona Leicester wakiwa dhaifu baada ya dirisha la uhamisho  ambapo katika dirisha hilo wamefanikiwa kumsajili mchezaji mmoja tu msimu huu wa joto ambae ni beki wa kati Wout Faes kutoka Reims ya Ufaransa.

 

Brendan Rodgers Achanganyikiwa

Wakati kwa upande mwingine wamewauza wachezaji muhimu ambao ndio walikuwa kwenye kikosi chao cha kwanza kama golikipa Kasper Schmeichel ambaye ameenda Nice ya Ufaransa, Wesley Fofana kwenda Chelsea. Brendan Rodgers anasema,

“Kwa heshima kubwa hatujapata msaada sokoni ambao timu ilihitaji”

Wakati timu nyingine zimesajili wachezaji bora Leicester atapitia hali mbaya labda afanye usajili kwenye dirisha dogo kwani upinzani uliopo kwenye vilabu ni mkubwa mno asipofanya hivyo kibarua chake kinaweza kuwaka moto.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.