Uingereza: Rasmi ligi daraja la kwanza (EFL) kurejea siku ya kesho baada ya kusimamishwa kwa siku takribani nne kufuatia kifo cha aliyekuwa Malkia wa Taifa hilo Elizabeth wa pili ambaye alifariki dunia siku ya Alhamisi akiwa na miaka 96.

EFL Kurejea Jumanne

 

EFL ilisimamishwa siku ya Ijumaa ambapo siku hiyo kuna mechi mbili zilitakiwa zipigwe na miongoni mwa mechi hizo  ni Norwich dhidi ya Burnley, lakini baadae ikatoka taarifa nyingine kuhusu kuzisimamisha ligi za daraja la kwanza zote pamoja na ligi kuu kwaajili ya kutoa heshima kwa Malkia. Lakini michuano ya klabu bingwa UEFA na EUROPA ziliendelea kama kawaida ili kuepusha kuharibu ratiba ya michuano hiyo na muda pia kuonekana hautoshi lakini pia michuano hiyo kuhusisha mabara mbalimbali.


Malkia huyo ambaye ameweka historia katika nchi ya Uingereza kuwa mtawala aliyetawala kwa muda mrefu takribani miaka 70 akikalia kiti hicho cha ufalme toka alipokuwa na miaka 27 na sasa kiti hicho amekabidhiwa mtoto wake Charles wa tatu akiwa na miaka 73.

 

EFL Kurejea Jumanne

Sasa ligi hiyo ya EFL inatarajiwa kurejea kesho na mechi kuendelea kupigwa ambapo baadhi ya mechi ambazo zinatarajiwa kupigwa kesho ni Blackburn Rovers dhidi ya Watford, Swansea dhidi ya Sheffield United, Hull City dhidi ya Stoke City, hizo ni baadhi ya mechi ambazo zitapigwa kesho na nyingine kuendelea siku ya Jumatano.

 


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa