Kocha Mkuu wa Geita Gold Fred Minziro alisema kuwa timu yake inatengeneza nafasi nyingi sana lakini wanashindwa kuzigeuza kuwa magoli, ila ipo siku watamfunga mtu goli 3 mpaka 5.

Kocha Mkuu wa Geita Gold Fred Minziro alisema kuwa timu yake inatengeneza nafasi nyingi sana lakini wanashindwa kuzigeuza kuwa magoli, ila ipo siku watamfunga mtu goli 3 mpaka 5.

“Mechi ilikuwa yenye ushindani, ukiangalia Hilal walikuwa Nyumbani lakini sisi tulitengeneza nafasi nyingi kuliko wao, lakini tulipoteza mchezo na tutajipanga kwa mchezo ujao”

“Mbali ya kukosekana kwa George Mpole lakini nawaambia kila siku vijana wangu, utulivu na umakini unapokuwa umeingia kwenye eneo la 18, ila vijana wetu na watanzania kwa ujumla huwa tunakosa utulivu na uamkini, lakini kwa jinsi tunavyocheza na kutengeneza nafasi kuna siku tutamfunga mtu goli 3 mpaka 5”. Minziro Kocha wa Geita Gold.

Kocha Mkuu wa Geita Gold Fred Minziro alisema kuwa timu yake inatengeneza nafasi nyingi sana lakini wanashindwa kuzigeuza kuwa magoli, ila ipo siku watamfunga mtu goli 3 mpaka 5.

Timu ya Geita Gold ilicheza mchezo wake wa mkondo wa kwanza wa Ligi ya Shirikisho barani Afrika wakiwa ugenini nchini Sudan dhidi ya Hilal Al Sahil na kupoteza kwa goli 1-0. Wanasubiri mchezo wa mkondo wa pili wa marudiano Nchini Tanzania.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa