Wakati Rais wa TFF, Wallace Karia akieleza kwamba hajui aliyerusha video ikimuonyesha amekwepa kusalimiana na kocha wa Geita Gold, Fred Minziro, amesema video hiyo imetengenezwa kwa lengo la kumchonganisha na kiongozi huyo wa soka nchini.

minziro

“Sijui aliyeiposti alikuwa na maana gani, muulize Minziro atakueleza ukweli,” amesema Karia.

Minziro alipoulizwa alisema ni video ambayo imetengenezwa kwa nia ovu ya kumchonganisha na Karia.

“Hivi Karia akatae kunipa mkono kwa sababu gani? ukiachana tu na kuwa rais wa mpira ni rafiki yangu na sijawahi kutofautiana naye, ni watu tu wameamua kuitengeneza kwa nia ovu ya kunichonganisha naye,” amesema.

Amesema alipokuwa jukwaani jana, Karia alimwambia ageuke ili apigwe picha na waandishi wa habari.“Kama angekuwa ananichukia angeniambia hivyo?,” alihoji Minziro na kubainisha kwamba hata leo asubuhi ameongea na Karia.

“Sina ugomvi na Karia, ni rafiki yangu tangu nacheza mpira na hata leo asubuhi nimezungumza naye, ni watu tu wanatengeneza vitu vya ajabu ajabu ili kuchonganisha wengine,” amesema.

Amesema kama kuna mtu amemsema vibaya Karia baada ya kuangalia video ile basi amemuonea, kwa kuwa ni video ambayo anadai imetengenezwa ili ionekane Karia hakumpa mkono wakati si kweli.


MAANA KAMILI YA USHINDI KATIKA KASINO ZA MERIDIANBETI NI PAMOJA NA MCHEZO WA PANDA PANDA.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Panda Panda na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Gomes, Gomes : Sitafanya Usajili wa Kutisha., Meridianbet

CHEZA HAPA

3 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa