Mshambuliaji wa Inter Milan Romelo Lukaku ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa ligi ya Italia Serie A kwa mwaka 2021 baada ya tuzo kutangazwa na uongozi wa Serie A baada ya ligi hiyo kutamatika hivi karibuni.

Msimu huu ulikuwa mzuri sana kwa Lukaku pamoja na Inter Milan Kwa ujumla. Akiwa kama mshambuliaji Lukaku alihusika kwenye magoli 34 ya Inter Milan, huku akifunga 24 na kutoa pasi 10 za usaidizi wa magoli.

Lukaku amecheza mechi 36 na ameisaidia timu yake kuchukua ubingwa wa Serie A. Mchezaji huyu alikuwa akichuana na Ronaldo kwenye tuzo ya mchezaji bora wa Serie A, huku Ronaldo akichukua tuzo ya mshambuliaji bora akiwa amefunga magoli 29.

Wachezaji wengine waliojinyakulia tuzo nyingine ni pamoja na, Dusan Vlahovic aliyeshinda tuzo ya mchezaji bora kijana, Nicolo Barrela akiwa kama kiungo bora wa Serie A, Christian Romero ameshinda tuzo ya beki bora pamoja na Gianluigi Donnarumma akichukua tuzo ya kipa bora.


MAANA KAMILI YA USHINDI KATIKA KASINO ZA MERIDIANBETI NI PAMOJA NA MCHEZO WA PANDA PANDA.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Panda Panda na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Gomes, Gomes : Sitafanya Usajili wa Kutisha., Meridianbet

CHEZA HAPA

3 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa