Georginio Wijnaldum Azungumzia Hatma Yake

Georginio Wijnaldum ametoa mwanga juu ya hatma yake katika mchakato wa kukamilisha uhamisho kwenda Barcelona.

Nyota huyu mwenye uraia wa Netherlands alishawaaga Liverpool wiki iliyopita na anaelekea kuwa wakala huru mwezi ujao.

Wakala wa Georginio Wijnaldum anaripotiwa kuonekana Barcelona wiki iliyopita, lakini pia Bayern Munich wamekuwa wakihusishwa na saini yake.

Georginio Wijnaldum

Akizungumzia juu ya uwezekano wa kuhamia kwake Barcelona, wakati akitimiza mahukumu yake ya kimataifa na Netherlands, Wijnaldum hakutaka kuzungumza mengi;

“Bado hauwezi kunipongeza kwa hilo. Bado siwezi kuzungumza juu ya hilo. Bado suala halijaisha, hivyo hakuna habari yoyote. Tutaona itakuwaje.”

 

“Bado niko bize kutoa salamu zangu za kwaheri Liverpool. Bado najihisi ugumu fulani, nimepewa salamu za kuagwa zaidi kuliko wachezaji wengine walivyopewa hapo kabla.” –

 

Georginio Wijnaldum

Nyota huyu amesema pia kwa sasa hawezi kuweka wazi sababu ya yeye kuondoka klabuni hapo, lakini anajua ukweli utakuwa bayana tu. Isipokuwa kwa sasa klabu inapswa kupambana na ukweli kuwa anaondoka.


MAANA KAMILI YA USHINDI KATIKA KASINO ZA MERIDIANBETI NI PAMOJA NA MCHEZO WA PANDA PANDA.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Panda Panda na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Gomes, Gomes : Sitafanya Usajili wa Kutisha., Meridianbet

CHEZA HAPA

3 Komentara

  Hatarii

  Jibu

  Hatari sana

  Jibu

  Kazi ipo

  Jibu

Acha ujumbe