Mshambuliaji Gabriel Jesus wa Manchester City atasalia nje kwa majuma matatu kuuguza jeraha la mguu alilolipata katika mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) iliyowakutanisha na Wolves uwanjani Molineux mnamo Septemba 21, 2020.
Shirikisho la Soka la Brazil limethibitisha kwamba Gabriel Jesus, 23, ameondolewa kwenye kikosi cha Brazil kilichotazamiwa kuvaana na Bolivia na Peru kwenye mechi zijazo za kufuzu kwa Copa America 2021.
Licha ya kupata jeraha katika dakika ya 66 wakati akichezea City dhidi ya Wolves, Jesus alisalia uwanjani kwa kipindi kizima cha dakika 90 na akafunga bao katika ushindi wa 3-1 waliouvuna.

Kuumia kwa Gabriel Jesus ni pigo kubwa kwa City ambao pia watakosa huduma za mshambuliaji Sergio Aguero kwa kipindi cha majuma saba yajayo kwa sababu ya jeraha la goti.
βManchester City waliwasiliana na daktari wa timu ya taifa ya Brazil, Rodrigo Lasmar, na kumfahamisha kuhusu ukubwa wa kiwango cha jeraha linalouguzwa na Jesus,β ikasema sehemu ya taarifa ya Shirikisho la Soka la Brazil (CBF).
Brazil watavaana na Bolivia mnamo Oktoba 9, 2020, kabla ya kushuka dimbani kupepetana na Peru mnamo Oktoba 13, 2020.
Manchester City watakuwa wenyeji wa Leicester City katika mchezo wa Ligi ya EPL utakaochezwa uwanjani Etihad.

Manchester City inatarajiwa kuendeleza rekodi nzuri ambayo imewashuhudia wakiibuka na ushindi katika mechi 10 na kuambulia sare mara moja katika jumla ya michuano 11 iliyopita uwanjani Etihad.
Tangu 1989-90, Manchester City hawajapoteza shindano lolote la mwanzo wa msimu uwanjani Etihad. Hiyo ni rekodi waliyoiendeleza mnamo Septemba 24, 2020 kwa kuwabandua Bournemouth kwenye raundi ya tatu ya Carabao Cup kwa kichapo cha 2-1.
FURAHIA KASINO YA MTANDAONI
Tembelea ardhi ya maajabu ushangazwe na mengi ikiwa ni pamoja na urahisi wa kujipatia utajiri kupitia Kasino ya Meridianbet.


felister
get well soon Gabriel
Sauda
Pole yake
Rehema
Pole sana
aisha
Gabriel pole sana kwa kupata jelaha ila utapona ndio mpira huo
Nasra
Pole yake
Caroline
Pole Sana Gabriel
Elika
Dah tumuombe ili aweze kurudi mchezoni
Rose kapinga
Ajali kazini
Lydia Emmanuel Magoti
Duu pole yake hajali kazn mzee baba utakuwa sawa tuu
Tatu
Da man city wamepata pigo kwa mchezaji wao
Dorophina
Pole yake gabriel
Adelta
Pole Sana brother
Mwajumah
Duuh pole yake
Ernest
Pep anakibarua hapa kwenye upande wa foward line. Muda huu ndio anauona umuhimu wa Mahrez
Zeiyana
Habari mbaya kwa mashabiki wa man city
Angelina
Getwellsoon
Aziza mushi
Pole Sana.
Hidaya
So sad
Fatina mfigi
Duuh pole
Samiah
Pole yake
Gabriel
Pengo kubwa sana kwa club ya man city
Hopemwaikuka
I feel sorry for him
Venerose
Pole sana
Issa
City wamepata pengo kubwa san
Sabrina
Dah pole sana namuombea apone ili arudi mchezoni
Rehema
Pole
Theonestina
Pole yake
Amiri Kayera
Injury mbaya kapata
Mariam mtandama
Pole
Latifa juma mohamed
Getwell soon.
Saupha mohamed
Pole sana
Fatuma kasomo
Pole yake
Theckla
Pengo kubwa kwa man city
Khadija
Pole sana
Janeflora malisa
Dah ‘ pol sn
Mwanahamisi
Pole yake
Povel
Get well soon ππΌππΌ
magdalena
pole sana gabriel utakuwa sawa
Salma ngende
Pole yake
Neema
Pole yake
Shani
Majeruh ya mara kwa mara yanamfany awe nje ya uwanja kwa muda mrefu
David Pere
Kuumia kwa Gabriel Jesus ni pigo kubwa kwa City ambao pia watakosa huduma za mshambuliaji Sergio Aguero kwa kipindi cha majuma saba yajayo kwa sababu ya jeraha la goti.