Borussia Dortmund waliduwazwa na FC Augsburg kwa kichapo cha 2-0 katika mechi ya Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga) iliyohudhuriwa na takriban mashabiki 6,000 uwanjani WWK Arena mnamo Septemba 26, 2020.
Felix Uduokhai aliwaweka wenyeji Augsburg kifua mbele kunako dakika ya 40 baada ya kushirikiana vilivyo na Daniel Caligiuri. Bao hilo lilikuwa la kwanza kwa Uduokhai kufunga tangu 2017.
Caligiuri alifungia Augsburg bao la pili katika dakika ya 54 alipokamilisha krosi ya Florian Niederlechner aliyemwacha hoi beki Thomas Meunier wa Dortmund.

Ingawa chipukizi Erling Braut Haaland alijitahidi sana kuwarejesha Dortmund mchezoni, ushirikiano wake na Jadon Sancho anayewaniwa na Manchester United haukuzalisha matunda yoyote na mashuti yake mawili yalipanguliwa kirahisi na kipa Rafal Gikiewicz.
Augsburg, ambao sasa wamepata ushindi katika michuano miwili ya ufunguzi wa msimu huu, walimiliki asilimia 20 pekee ya mpira na mabao mawili waliyoyapata yalitokana na nafasi mbili za pekee ambazo walipata langoni pa Dortmund katika dakika 90 za kwanza.
Alfred Finnbogason nusura awafungie Augsburg mabao mawili ya ziada mwishoni mwa muda wa majeruhi ila akanyimwa fursa na kipa Roman Burki.

Mechi hiyo ilikuwa ya tatu kwa chipukizi raia wa Uingereza, Jude Bellingham, 17, kuchezea Dortmund tangu ajiunge nao kutoka Birmingham City. Fowadi huyo aliondolewa uwanjani katika dakika ya 60.
Kwingineko, Bayer Leverkusen na RB Leipzig waliambulia sare ya 1-1.
FURAHIA KASINO YA MTANDAONI
Tembelea ardhi ya maajabu ushangazwe na mengi ikiwa ni pamoja na urahisi wa kujipatia utajiri kupitia Kasino ya Meridianbet.


Ernest
Jana Dortmund walilewa kidogo na ubora wa timu yako walidhani wataweza fanya comeback kama kawaida yao lakini kilichowakuta ni Aibu tupu
Fatina mfigi
Pole yao!
Asia Abdy
Sikutegemea dah
Sauda
Dortmund hawana jipya
Rose kapinga
Mambo yalikua motooo
Lydia Emmanuel Magoti
Hiyo inaitwa kuizalau timu kwaio Dortmund wakiizalau Augsburg ndomana matokeo yalikuwa vile
Venerose
Tatizo Dortmund walijiamini sana
Caroline
Nilijua tu Dortmund wataumia
Zeiyana
Toka mapunziko ya korona mambo yamekua yanabadilika badilika hii haibu kweli kwa timu kubwa kama Dortmund
Tatu
Dortmond walizidiwa na watoto wadodo awakujipanga
Rehema
Dortmund wako vizuri
felister
kwa matokeo aya sidhani kama kuna mtu atakua amekula mkeka dah inaniuma kwa Dortmund kunichania mkeka 😭
Elika
Dah wako vizur
Mwajumah
Tatizo Dortmund walijiamin sana
aisha
Duuh imeniuma sana sijui walikwama wapi
Nasra
Dortmund kiboko
Mwajumah
Dortmund wako vizuri
Adelta
Dotmund pole Sana lakini mpira hautabiriki Ila ongezeni juhudi na kuimarisha klabu
Angelina
Dortmund jana wamezingua
Aziza mushi
Duh Dortmund wameniangusha.
Hidaya
Dotmund wamechana jamvi
Samiah
Dotmund wamenikosesha pesa
Gabriel
Mtanange n mkal sana 👍
Juliana Alex
Jamani
Hopemwaikuka
Mmetisha washkaj
Issa
Dortmund ni mech ambayo walipoteana vibaya
Sabrina
Duuh hatari sn dortmund wameyumbaa
Theonestina
Duuuh
Amiri Kayera
Dortmund walipoteana
Mariam mtandama
Duuuh
Latifa juma mohamed
Pole yao
Saupha mohamed
Nomaaa
Fatuma kasomo
Duh
Theckla
Haikuwa mechi nzuri kwa Dortmund
Khadija
Dortumund nawakubali sana
Janeflora malisa
Mambo mazur
Mwanahamisi
Pole yao
Povel
Wametu chania mikeka yetu dormund
magdalena
dortmundi waliishi kwa kukalili na bora walivyopokea kichapo
Dorophina
Dortmund walijisahau sana wakajua watoto wadogo watawaweza mwisho wa siku wameambulia kichapo
Salma ngende
Awana jipya hao
Neema
Dortmund poleni kwa kwelii
David Pere
Jana Dortmund walilewa kidogo na ubora wa timu yako walidhani wataweza fanya comeback kama kawaida yao lakini kilichowakuta ni Aibu tupu