Gilmour Asajiliwa Brighton

Klabu ya Brighton ambayo ipo chini ya kocha Graham Potter wamekamilisha usajili wa mchezaji kutoka Chelsea Billy Gilmour. Billy Gilmour ambaye ana umri wa miaka 21 anacheza katika nafasi ya kiungo wa kati.

Gilmour Asajiliwa Brighton

Brighton ambayo makazi yake yapo pale Amex Stadium wamemnunua Gilmour kwa ada ya £9M na huweza akacheza mechi ijayo siku ya jumapili ambayo itawakutanisha Brighton dhidi ya Leicester ambapo watakuwa nyumbani.

Msimu uliopita Gilmour alitolewa kwa mkopo katika timu ya Norwich City iliyokuwa imepanda daraja  ambapo alicheza msimu mmoja na baadae timu hiyo ikashuka tena  daraja. Mchezaji huyo wa Scotland alikuwa akiwaniwa na Brighton kabla ya kufungwa kwa dirisha hili kubwa la usajili ambapo ilikuwa inaonekana kama kuna ugumu wa mchezaji huyo kuondoka kutokana na Chelsea kuwa na uhitaji mkubwa wa kiungo, Lakini baadae ikawezekana kwenda Brighton.

 

Gilmour Asajiliwa Brighton

Inawezekana kuwa Brighton wamefanya usajili mzuri kwani kiungo huyo ana uwezo mkubwa na huenda akawasaidia akipatiwa nafasi ya kucheza kutokana na kuwa Brighton ni timu ya daraja lake hivyo hakutakuwa na presha kubwa kwani timu hiyo pia inaleta ushindani mkubwa katika ligi kuu England.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.