Bernardo Silva alisema Manchester City ilipokea ofa moja pekee rasmi kwa ajili yake kwani kiungo huyo atasalia na klabu hiyo licha ya kuhusishwa kusajiliwa na baadhi ya vilabu vikubwa barani ulaya.

- Ni Timu Zipi Hizo Zilizomuhitaji?
Kiungo huyo alikuwa akihusishwa na Barcelona na Paris Saint-Germain majira yote ya joto, lakini kiungo huyo anasema ni ofa moja pekee iliyowahi kutolewa mwishoni mwa dirisha la usajili.

- Yeye Mwenyewe Anasemaje?
“Ni moja ya vilabu vitatu vya juu ulimwenguni kwa sasa labda kwa hivyo nisingeweza kuwa bora hapa. Ni klabu ninayotaka kuwa nayo na nina furaha,”

Silva alisema. “Haukuwa uamuzi mgumu kwa sababu hakukuwa na ofa. Kulikuwa na ofa moja kutoka kwa timu moja, sio zaidi ya hiyo, kwa hivyo ilikuwa rahisi sana kwangu na kwa klabu kwa sababu ofa pekee iliyokuja ilikuja kuchelewa hivyo kwa klabu kupata mbadala wake haingekuwa rahisi.”

Manchester City sasa wataweza kumbakiza kiungo wao nyota, ambaye ameanza katika kila mechi kati ya mechi tatu zilizopita za Manchester City, akifunga bao moja na kuongeza pasi ya mabao “Assist” katika kipindi hicho.


