James Garner Atua Everton

Klabu ya Everton yenye makazi yake pale St. Goodison Park wamekamilisha usajili wa James Garner kwa dau la £15M kutoka Manchester United. Garner alitokea kwenye akademi ya United ambapo msimu uliopita aliutumia akiwa Nottingham Forest kwa mkopo kabla hawajapanda ligi kuu.

 

James Garner Atua Everton

James anacheza katika nafasi ya kiungo wa kati anaenda kuungana na kikosi hicho kinachonolewa na kocha mkuu Frank Lampard, ambao bado wanajitafuta kunako ligi kuu ya Uingereza kutokana na kuwa na mwendelezo mbovu wa matokeo wanayoyapata.

Everton msimu uliopita walinusuruka kushuka daraja na sasa wameanza vibaya msimu kwani hakuna hata mchezo mmoja wamefanikiwa kupata alama tatu, wamepata sare tatu na wamepoteza michezo miwili huku wakiwa katika nafasi ya 17 kwenye msimamo wa ligi.

James Garner Atua Everton

Ikumbukwe kuwa kesho siku ya jumamosi wanaenda kucheza dhidi ya Liverpool ambayo ni Marseyside derby ambapo msimu uliopita walipokutana Everton alipigwa nje ndani na majogoo na sasa ni msimu mwingine ambapo inabidi ajitathmini kwani biashara ni asubuhi. Ujio wa James  Gueye na wengine pia unaweza kuongeza kitu kwenye tomu hiyo ambayo bado haipo. Wataweza kweli kupata alama tatu dhidi ya Klopp?

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.