Mshambuliaji wa Manchester City Erling Braut Haaland anashikilia nafasi ya kwanza kati ya watano kwa wachezaji waliofunga mabao mengi baada ya michezo mitano ambayo wamecheza toka ligi ya Uingereza ilipoanza msimu huu wa 2022/2023.

Haaland ambae amesajiliwa msimu huu na Pep Guardiola kutoka Borrusia Dortmund ni mchezaji wa timu ya Taifa ya Norway na City. Mpaka sasa ndani ya michezo mitano aliyocheza amefunga mabao 9 huku akitupia hattrick mara mbili mfululizo na akiwa ndiye mchezaji wa kwanza kufanya hivyo msimu huu.
Nafasi ya pili inashikiliwa na Aleksandar Mitrovicanayechezea Fulham ambayo imepanda daraja msimu huu. Mchezaji huyo amepachika mabao 5 mpaka sasa kwenye klabu yake hiyo huku wakiwa wamepoteza mchezo mmoja tuu.

Kwa upande wa nafasi ya tatu wamefungana wachezaji watatu ambao wamefunga mabao manne. Harry Kane anayecheza katika klabu ya Tottenham Spurs, Rodrigo Moreno anayecheza Leeds, pamoja na Willfred Zaha kutoka Crystal Palace.

