Uefa Kuvichungaza Vilabu 18 .

Uefa shirikisho la soka barani ulaya litavichunguza vilabu 18 kwenye sheria ya matumizi ya pesa inayojulikana kama (Financial Fair Play).

Shrikisho hilo limeppanga kuvifuatilia vilabu hivyo kama vimefata sheria hiyo kwa ufasaha bila kuivunja na endapo itabainika vilabu vimevunja sheria watakumbwa na adhabu ya kufungiwa kusajili na kupigwa faini ila itategemeana na ukubwa wa uvunjifu wa kanuni.

Vilabu ambavyo vipo kwenye uchunguzi huo ni vilabu vya Borussia Dortmund,Barcelona,Fc Basel,Union Berlin, Fenerbahce,Feyernoord,Leicester city,Manchester city,Lyon,Rangers,Real betis,Royal antwerp,Sevilla,Lazio,Napoli,Trabonzspor,Wolfsburg, pamoja na West ham united.

Vilabu kadhaa vishawahi kukubwa na hatia ya kufanya matumizi mabaya ya pesa na kupewa adhabu ya kufungiwa usajili na kupigwa faini baadhi ya vilabu hivo ni Chelsea,PSG, and Manchester city.

Sheria hii ipo kwajili ya kusimamia matumizi sahihi ya vilabu vya soka duniani na kuhakikisha wanatumia kulingana na wanachoingiza ikibainika klabu imefanya matumizi makubwa kuliko kiwango inachoingiza basi hapo itakumbana na adhabu kutoka Uefa au Fifa.

 

Acha ujumbe