Emiliano Martinez Akosa Usingizi.

Golikipa namba moja wa timu ya Aston Villa Emiliano Martinez  amesema kuwa amekuwa akikosa usingizi kutokana na jinsi ambavyo wameanza vibaya msimu huu wa ligi kuu. Alikiambia chombo cha habari cha michezo Uingereza.

 

Emiliano Martinez Akosa Usingizi.

Emiliano amekiri kuanza kwao vibaya kwa msimu wa ligi kuu ya Uingereza kunamfanya anakosa usingizi. Anasema hata wakishinda na akiruhusu goli, hakulala kabisa walipofungwa na Arsenal, anapata shida kupata usingizi.

Anapitia wakati mgumu wanapopoteza mchezo hiyo yote ni kutokana na mapenzi aliyonayo na klabu hiyo hivyo basi hukaza buti kwani hujisikia vibaya kuona watoto wakiwa wamevaa jezi ya klabu yake huku wakimuimba jina lake hapo ndipo humfanya aipende klabu hiyo na asalie hapo, huku akikosa usingizi.

Ameongezea kwa  kusema kuwa wachezaji wanatakiwa kuwajibika kwa hali hiyo ya sasa  na sio kocha wa timu hiyo Steven Gerad.

Emiliano na timu yake mpaka sasa wamepokea vichapo vinne kikiwepo kile cha mwisho walichopokea katikati ya wiki kutoka kwa vinara wa ligi Arsenal, ambapo walipoteza kwa mabao 2-1 kitu ambacho kimewafanya wawe chini kabisa ya msimamo ambapo wapo nafasi ya 19 kutokana na matokeo hayo.

 

Emiliano Martinez Akosa Usingizi.

Leo hii watakuwa nyumbani kuwaalika vijana wa Guardiola Manchester City  ambao wapo nafasi ya pili kwenye msimamo na wamekuwa bora sana hasa katika eneno la ushambuliaji kwani ndio timu inayoongoza kwa kufunga mabao mengi mpaka sasa. Matokeo ambayo wanayapata Aston Villa  hayo yanaweza kusababisha kocha wao kibarua chake kuota nyasi.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.