Golikipa wa Aston Villa, Emiliano Martinez, amesaini mkataba mpya wa miaka 5 na nusu kuendelea kutumikia klabu hiyo kule Villa Park.
Martinez alijiunga na Aston Villa Septemba 2020 na, ameitumikia Villa kwa michezo 58 akiisaidia Villa kupata clean sheet 15 kwenye msimu wake wa kwanza kule Villa Park.
Akiwa tayari ametwaa kombe la Copa America na Timu yake ya Taifa (Argentina), Emiliano analengo la kutwaa mataji akiwa na Aston Villa baada ya kushindwa kufanya hivyo na Arsenal wakati akiitumikia timu hiyo.
Akizungumza baada ya kusaini mkataba mpya, Martinez amesema;
Kabla sijaingia uwanjani, huwa ninaona picha ya Kombe la Ligi ya Mabingwa na FA, huko ndio ninakotaka kwenda. Ninataka kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa nikiwa na Villa, niingie Wembley kucheza fainali ya FA au Carabao Cup. Ndio maana nimejifunga kwa miaka 5 na nusu na klabu hii ili nifike huko.
Villa watakua uwanjani wikiendi kuchuana na Everton katika muendelezo wa EPL.
Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.
CHEZA HAPA