Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Ubelgiji na klabu ya Real Madrid Edin Hazard aanza leo kwenye kikosi cha kwanza ambacho kinaanza dhidi ya Mallorca ambapo hiyo ni baada ya kukaa miezi 9 bila kuanza kwenye kikosi cha kwanza cha  Carlo Ancelloti.

 

Hazard Aanza Kwenye Kikosi

Hazard ambaye ana umri wa miaka 31 toka ajiunge na klabu hiyo akitoka Chelsea amekuwa akisumbuliwa na majeraha hivyo kutopata muda mwingi wa kucheza hata kupata nafasi ya kuanza katika kikosi hicho imekuwa shida kwake kutokana na kuwepo watu wenye kupambania namba wengi.

Real Madrid ambao ni mabingwa watetezi wa ligi hiyo wamekuwa na mwendelezo mzuri wa matokeo kwenye ligi kwani mpaka sasa hawajapoteza mchezo wa aina yoyote, na Benzema amekuwa mfungaji bora wa klabu hiyo ambapo hataanza leo kwenye kikosi kutokana na majeraha aliyoyapata kwenye mchezo uliopita.

 

Hazard Aanza Kwenye Kikosi

Hazard na wenzake wakimaliza mchezo huu watacheza mchezo wa klabu bingwa Ulaya ambapo watawakaribisha RB Leipzig katika mchezo wao wa pili. Mchezo wa kwanza walishinda ushindi mnono dhidi ya Celtic ugenini, huku kwa upande wa RB Leipzig akipoteza kwa mabao 4-1 dhdi ya Shakhtar Donetsk, lakini sasa wana kocha mpya anaekinoa kikosi hicho ambae ni kocha wa zamani wa Dortmund Marco Rose na ametoka kushinda mechi yake ya kwanza dhidi ya Dortmund.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa