Bondia Mtanzania Ibrahim Class ashinda kwa KO katika raundi ya tisa hapo jana katika mshindano ya ngumu ambayo yameanzishwa na muwekezaji wa Simba Mohamed Dewji maarufu kama (Mo Boxing) ambapo bondia huyo alikuwa akizitwanga na Alan Pina kutoka Mexico.

 

Ibrahim Class Ashinda kwa KO

Ibrahim ameshinda katika shindano ambalo halikuwa na ubingwa ambalo limefanyika jijini Dar es salaam, ambapo licha ya pambano hilo kulikuwa na mapambano mengine pia ambayo yalifanyika na watu walihudhuria kwa wingi.

Pambano hilo limeishia raundi ya 9 baada ya Alan Pina kupigwa ngumi nzito iliyomfanya aanguke chini na kudaiwa kupoteza fahamu kitendo kilichofanya atolewe ulingoni kwa haraka zaidi ili kupatiwa huduma ya kwanza.

 

Ibrahim Class Ashinda kwa KO

Baada ya kutolewa nje kwaajili ya huduma ya kwanza, taarifa zilitoka na kusema bondia huyo Mmexico anaendelea vizuri na yuko fiti. Mchezo huu sasa umekuwa pendwa sana kiasi cha watu wengi kuhudhuria kushuhudia ngumi.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa