KUELEKEA mchezo wao wa ligi dhidi ya Ruvu Shooting, benchi la ufundi la Yanga limefunguka kuwa wanatambua mchezo huo utakuwa mgumu lakini wanahitaji pointi tatu ili kuendeleza rekodi ya kutopoteza mchezo.
Yanga tangu msimu wa 2021/22 mpaka sasa haijawahi kupoteza mchezo wowote wa ligi na kufanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu, Shirikisho la Azam na Ngao ya jamii.
Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze amesema kuwa “Tunaendelea na maandalizi na tunaenda kwenye huo mchezo kwa tahadhari kubwa kwani tunajua kwamba mchezo huo utakuwa mgumu sana.
“Ruvu Shooting hata msimu uliopita walitusumbua sana na walisababisha tukagawana pointi kule kigoma lakini kwa sasa tunahitaji zaidi ushindi.”
Mchezo huo wa ligi kuu unatarajiwa kupigwa Oktoba 3 mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.
Baada ya mchezo huo wananchi watakwenda kucheza mchezo wa raundi ya kwanza dhidi ya klabu ya Al-Hilal ya Sudani oktoba 8 katika Uwanja wa taifa jijini Dar-es-salaam.