Yanga Yapata Mdhamini Mwingine

Klabu ya wanawake “Yanga SC Princess” imeingia makubaliano ya udhamini na kampuni ya vinywaji ya Watercom kupitia kinywaji chao cha Jembe Energy kwa kipindi cha mwaka mmoja wenye thamani ya Shilingi Milioni 120 sawa na Milioni 10 kwa kila mwezi, pia kampuni hiyo itakuwa inatoa Lita 1500 kwa klabu hiyo kila mwezi.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka klabu hiyo ilithibitisha kuingia mkataba wa mwaka mmoja na kampuni hiyo.

 

Yanga Yapata Mdhamini Mwingine

“Timu ya Yangasc Princess leo imeingia mkataba na Kampuni ya Watercom, kama mdhamini/mshirika wetu kupitia kinywaji chao cha Jembe Energy kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Akizungumza katika mkutano wa Waandishi wa Habari Rais wa Klabu ya Yanga SC, Eng. Hersi Said alisema,

“Huu ni muendelezo wa ajenda yangu kubwa ya kuimarisha timu kiuchumi, na kwa kupitia mkataba huu tunaendelea kuimarisha hali yetu ya kiuchumi ili kuwa imara zaidi. Kwa miaka mingi vilabu vyetu vimekuwa vikikumbana na adha mbalimbali za kiuchumi na hii inatokana na kukosekana mikakati imara ya kuwashawishi wadhamini. Unapokuwa na uongozi imara inasaidia hata washirika wengine kuja kuwaunga mkono. Unapokuwa na timu imara inavutia wadau wengi kuja.

“Mkataba wetu una thamani ya Tsh milioni 120 sawa na milion 10 kwa mwezi. Vile vile watercom watatoa lita 1500 kwa Klabu yetu kila mwezi.

 

Yanga Yapata Mdhamini Mwingine

Nae Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Klabu hiyo Andre Mtine alionesha hali ya kufurahia hatua hiyo.

“Leo ni siku muhimu sana kwetu kwenye maendeleo ya mpira. Ninajivunia kuona nasaini mkataba mpya kwa niaba ya Klabu. Hii ni hatua kubwa sana na inaonesha kwa jinsi gani klabu hii imejipanga kuboresha masuala ya kiuchumi” Andre Mtine Mtendaji mkuu Young Africans SC.

 

Yanga Yapata Mdhamini Mwingine
Huu unakuwa ni muendelezo kwa klabu hiyo wa kuingia udhamini na makapuni tofauti ambapo hapo nyuma waliingia mkataba na kampuni ya GSM wa Shilingi Bilioni 10 kwaajili ya usambazaji wa Jezi na vifaa vyenye chapa ya klabu hiyo.

Acha ujumbe