KIKOSI cha KMC kesho jumamosi kitashuka katika dimba la Majaliwa, Lindi kumenyana na Namungo ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu.

KMCTimu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni iliwasili jana alhamis usiku na imefanya mazoezi ya mwisho leo kwenye uwanja huo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa “Kikosi chetu chini ya Kocha Mkuu Thierry Hitimana tayari kilifanya maandalizi ya kutosha tangu Dar na mazoezi ya leo yanalenga kuwaweka sawa wachezaji kutokana na safari waliyokuwa nayo.

“Kwa upande wa hali za wachezaji wote wako vizuri na kwamba kila mmoja ana ari na morali ya kuhakikisha kwamba licha ya kuwa mchezo huo utakuwa na ushindani lakini KMC tunahitaji kupata matokeo mazuri kwakuwa mchezo huo upo ndani ya uwezo wa timu.

KMC“Tumekuja kutimiza kile ambacho tunakihitaji, mchezo utakuwa mgumu ila tumejipanga vyema kuwakabili wapinzani wetu, na tunajua kabisa wanatimu nzuri tunawaheshimu pia, ila mwisho wa siku sisi ni bora zaidi yao.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa