BAADA ya kumalizana na Coastal Union, kikosi cha Ruvu Shooting sasa kinajiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Yanga huku Kocha Mkuu, Boniface Mkwasa akisema kuwa hawataki kuruhusu mabao mengi kwenye mchezo huo.

asaliRuvu Shooting ambao tangu kuanza kwa msimu huu wamekuwa kwenye kiwango kizuri watawakabili mabingwa watetezi Yanga kwenye mchezo ujao wa ligi.

Mkwasa amesema kuwa Mipango ambayo wataingia nayo kwenye mchezo huo itatofautiana na ile ambayo waliitumia kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union.

“Mchezo utakuwa mgumu, tunajua Yanga wana rekodi nzuri tangu msimu uliopita lakini tutaingia na plani nyingine kwenye huo mchezo.

mkwasa“Tunajua kwa matokeo ya mchezo dhidi ya Coastal Union tutakuwa tumejitafutia matatizo kuelekea mchezo ujao lakini tunahitaji kuzipata pointi tatu au basi ikishindikana angalau moja lakini tutahakikisha wasitufunge magoli mengi.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa