Arsenal na klabu ya Tottenham Hotspurs kesho wanakwenda kumenyana katika mchezo wa dabi ya London kaskazini miongoni mwa dabi zenye mvuto na uhasimu mkali nchini Uingereza, Mchezo huo utakaopigwa saa nanena nusu mchana kwa saa za Afrika mashariki.

 

arsenalArsenal vinara wa ligi kuu Uingereza wakiwa na alama 18 katika michezo 7 wakishinda michezo sita huku wakifungwa mchezo mmoja huku klabu ya Tottenham wao wakiwa na alama 17 baada ya kushinda michezo mitano na kusuluhu michezo miwili wakiwa hajafungwa mchezo hata mmoja mpaka sasa latika ligi hiyo.

Mchezo unaovikutanisha vilabu hivi hua na uhasama mkali sana kwakua vilabu hivi vinatoka jiji moja lakini kubwa zaidi vinatoka ukanda mmoja kwa maana ya London kaskazini hivo wakikutana hua kunakua na mtanange mkali sana kutokana na uhasimu wao.

Klabu ya Arsenal ambao wameanza msimu huu vizuri wana nafasi ya kulipiza kisasi baada ya kufungwa tatu kwa bila walipokutana mara ya mwisho na kunyimwa nafasi ya kushiriki ligi ya mabingwa ulaya na mahasimu zao hao.

arsenalTimu zote zinaenda huku zikiwa na vikosi vyao kamili hivo kila timu ina uwezekano kushinda mchezo huo wa kesho katika dimba la Emirates.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa