Azam Fc matajiri wa Dar-es-salaam wamekumbana adhabu kutoka kwa maaskari magereza jijini Mbeya baada ya kuchezea kichapo kutoka kwa klabu ya Tanzania Prisons bao moja kwa bila.

azamAzam wanashindwa kupata alama tatu baada ya kupokea kichapo jijini Mbeya,klabu hiyo ni miongoni mwa timu zilizofanya usajili bora kabisa msimu huu katika ligi kuu ya NBC Tanzania lakini wamekua wakipata matokeo ambayo sio ya kufurahisha.

Klabu ya Tanzania Prisons yenyewe iliofanikiwa kuifunga klabu ya Azam kupitia bao la Jeremia Juma dakika ya 46 ya mchezo wao wamefanikiwa kupanda nafasi tatu kutoka nafasi ya 11 mpaka nafasi ya nane wakiwa na alama zao 7.

Wanalambalamba wao wakishuka kwa nafasi kutoka nafasi ya 5 mpaka nafsi ya 6 wakiwafungana alama na timu ya Singida Big Stars Singida wakiwa juu kwa tofauti ya magoli baada ya waoka mikate kucheza ,ichezo mitanohuku singida wakicheza minne.

azamLigi kuu ya Tanzania msimu huu imeonekana kua yenye ushindani mkubwa baada ya kila timu kuonekana kutokubali kupoteza mchezo kirahisi katika michezo yake.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa