Klabu ya Arsenal bado wana nia ya kutaka kumsajili Douglas Luiz na wanatumai wanaweza kufikia makubaliano ya bei nafuu kumnunua kiungo huyo wa Aston Villa mwezi Januari ili waweze kuimarisha kikosi chao.

 

Arsenal Wanatarajia Kupiga Dili la Luiz

The Gunners watafanya jaribio jingine la kumpata Luiz mwenye umri wa maika  24, wakati wa dirisha dogo la usajili la mwezi Januari kwa mujibu wa The Sun.

Dili mbili za siku ya mwisho zilishindwa kumshawishi Mbrazil huyo kutoka kwa kocha mkuu Steven Gerrad Aston Villa huku washika mitutu hao  wa London Kaskazini wakijaribu kuimarisha chaguzi za Mikel Arteta katikati mwa uwanja.

Luiz atakuwa amebakiza miezi sita pekee katika kandarasi yake katika viwanja vya Villa Park ifikapo Januari baada ya kukataa ofa nyingi za kuongeza muda wake wa kusalia kwenye kikosi cha Steven Gerrard.

 

Arsenal Wanatarajia Kupiga Dili la Luiz

Na Arsenal sasa wanatumaini ofa ya pauni milioni 15 chini ya pauni milioni 23 ambayo walikuwa tayari kulipa msimu wa joto  itawashawishi Villa kumuuza mchezaji huyo kwani hataki kusaini kandarasi ya kusalia klabuni hapo.

Kuumia kwa Thomas Partey kunamaanisha kuwa nyongeza katika eneo hilo inasalia kuwa kubwa kwa The Gunners, huku Arteta akiwa na hamu ya kuhakikisha kiwango chao cha mapema hakitoki. Ukosefu wa nafasi na kikosi cha Midlands kumemfanya Luiz, aliyechezeshwa mara tisa na nchi yake, kuchanganyikiwa na aliripotiwa kutaka kubadili mapema mwaka huu.

 

Arsenal Wanatarajia Kupiga Dili la Luiz

Mchezaji huyo anamfahamu Arteta tangu walipokuwa pamoja Manchester City, jambo ambalo linapaswa kuthibitisha motisha yake ya  kuzungumza na viongozi wa sasa wa Ligi Kuu ya Uingereza.

Arsenal ndio vinara wa ligi kuu ya Uingereza mpaka sasa ambapo mpaka sasa wamepoteza mchezo mmoja tuuh kwenye ligi na wikiendi hii watamkaribisha Tottenham katika Dabi yao ya London.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa