KIKOSI cha KMC chenye jumla ya wachezaji 20, Viongozi na Benchi la ufundi kimeondoka leo kuelekea Ruangwa, Lindi kwa ajili ya mchezo wa Ligi dhidi ya Namungo.

Akizungumzia hali ya kikosi, Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala alisema: “Tunakwenda kwenye mechi yenye ushindani, lakini tumejipanga vizuri, tunawafahamu vizuri Namungo, licha ya ushindani kuwa mkubwa lakini kama Timu tunakwenda kwa tahadhari Ili kuhakikisha kwamba tunapata ushindi.

Siku zote hakuna mchezo mwepesi, michezo yote inahitaji maandalizi ya kutosha, jambo ambalo kama timu tumelifanya hivyo tunamuomba mwenyezi Mungu atufikishe salama Ili tukapambane uwanjani kupata alama tatu muhimu.

“Kwa upande wa hali za wachezaji wote wameondoka wakiwa salama, wana hali nzuri, wanamorali zaidi ya kutafuta ushindi kwenye mchezo huo muhimu.

Mashabiki na watanzania wote ambao siku zote wanaisapoti timu ni jukumu la kila mmoja kuwaombea wachezaji afya njema ili kuhakikisha burudani ambayo wameonesha kwenye michezo minne iliyopita inaendelea dhidi ya Namungo”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa