KAZI imenza kwa Timu ya Taifa ya Tanzania ya Wasichana wa (U17) Serengeti Girls ambayo imeweka kambi kwenye mji wa Southompton wakijiandaa na mashindano ya kombe la dunia yatayofanyika mwezi ujao India.

Kikosi hicho kilichopo chini ya Bakari Shime, jana kilicheza mchezo wa kirafiki na klabu ya SFC Development Squad yah apo hapo Southompton na mchezo huo kumalizika kwa suluhu.

Shime alisema timu hiyo itakuwa na michezo mingine ya kirafiki kwenye kipindi hiki cha zaidi ya wiki moja ambacho watakuwa kwenye mji huo wakijiandaa na mashindano hayo.

“Kwanza tunashukuru Mungu kwa kuweza kusafiri salama na kuanza maandalizi yetu hapa London, tulianza progaramu yetu ya mazoezi mepesi kabla ya kucheza mechi yetu.

“Nafikiri tutakipata kile tunachotaka baada ya wiki moja na wachezaji watakuwa wameshakuwa tayari kwa asilimia 100 kwa mashindano hayo,” alisema Shime.

Serengeti wamepangwa kundi D na timu za Ufaransa, Japan na Canada. Mechi ya kwanza watacheza Oktoba 12 dhidi ya Canada, kisha Oktoba 15 watakipiga na Ufaransa, kabla ya kumalizana na Canada.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa