Antonio Conte kocha wa Tottenham Hotspurs ametoa maoni yake juu ya masuala ya kibaguzi baada ya mchezaji wake kubaguliwa katika mchezo wa kimataifa siku ya jumanne.

antonio conteKocha ametaka mashabiki hao wanaofanya vitendo vya kibaguzi wafungiwe maisha kujihusisha na michezo,kitendo hicho cha mchezaji huyo kubaguliwa kilikuja wakati mchezaji huyo anaitumikia timu yake ya taifa siku ya jumanne katika mchezo dhidi ya Tunisia na kukutana na kitendo cha kibaguzi na mashabiki baada ya kurushiwa ndizi katika mchez huo.

Richarlison alionesha kukerwa zaidi na kitendo hicho na kuhitaji hatua kali zichukuliwe kwa mashabiki hao huku akitilia shaka kama hatua hizo zitachukuliwa.

Huku wachezaji wenzake wakionesha kutofurahishwa na kitendo hicho na kupaza sauti hatua zichukuliwe kama ilivyo kwa nahodha wake katika klabu ya Tottenham Harry Kane ambaye amewaeleza Fifa kuchukua hatua kali kwa mashabiki hao kwani wachezaji wanapambana kila siku ubaguzi uishe lakini shirikisho lina nguvu zaidi ya kuweza kufanikisha hilo alidai Kane.

antonio conte“Nadhani tunapaswa kuchukua hatua nzuri dhidi ya tukio hilo Richy alicheza timu ya taifa na akafunga mabao, Kilichotokea ni cha kushangaza kwani mwaka 2022 kushuhudia tukio kama hilo ni aibu kwa kila mtu”Alisema Antonio Conte.

“Kwa hakika natumaini watu hawa watafungiwa kujihusisha na mpira kwa maisha yao yote” Ni hali ya kukatisha tamaa sana, kulazimika kutoa maoni kuhusu hili.Nataka kuchukua sehemu nzuri ya mchezo ambapo Richy akifunga mabao na kufurahi”alisema Antonio Conte

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa