MENEJA wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema kuwa kwa namna yoyote ile mchezaji wao raia wa Serbia Dejan Georgijevic hawezi kuachwa salama kwa kitendo alichofanya cha kukiuma misingi ya klabu hiyo.
Ahmed alisema, Dejan alikuwa na mkataba ambao umetimia kila kitu baina yake na Simba na alichofanya ni kinyume na utaratibu na kama kulikuwa na shida mahali hakupaswa kufanya alichofanya bali alitakiwa kufuata utaratibu ikiwemo kuzungumza na viongozi kwanza.
Ahmed alisema: “Dejan maarufu kama mlete mzungu hawezi kuachwa hivi hivi, lazima atachukuliwa hatua za kinidhamu na kisheria kwa sababu amekwenda kinyume na utaratibu wa klabu.
“Hauwezi mchezaji ambaye ni professional ukaondoka au kuvunja mkataba Instagram hata kama ni kweli utakuwa na madai na klabu yako. Kuna namna ya kufanya ikiwemo kuzungumza na viongozi au wawakilishi wako.
“Suala la Dejan lipo kwenye mikono ya sheria na wawakilishi wake tayari wameshafikishiwa taarifa na mambo yakishakaa sawa tutawapa ripoti.”
Dejan aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa amevunja mkataba na Yanga kwa kile alichodai ni kukiukwa kwa baadhi ya vipengele vya kimkataba na timu hiyo.