MWAMUZI ambaye anakumbukwa zaidi kutokana na kuchezesha mchezo wa ligi kuu kati ya Yanga na Azam, Ahmed Arajiga amelamba dili la kuchezesha mechi za kufuzu AFCON chini ya miaka 17.

mwamuziArajiga ataungana na Kassim Mpanga wote wakitokea Tanzania ambao wote kwa pamoja watakuwa na jukumu la kusimamia sheria 17 za mchezo wa soka katika michuano hiyo.

Kutokana na viwango bora vilivyoonyeshwa na waamuzi hao vimewashawishi mabosi wa CECAFA kuwateua kuwa miongoni mwa waamuzi watakaosimamia mashindano hayo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Shirikisho la Soka nchini (TFF), imeeleza kuwa “Mwamuzi wa kimataifa wa Tanzania, Ahmed Arajiga na Mwamuzi Kassim Mpanga wameteuliwa na CECAFA kuchezesha mashindano ya kufuzu AFCON U17 Kanda ya CECAFA yatakayofanyika Ethiopia.”

mwamuziIkumbukwe Timu ya Taifa ya Tanzania pia ni miongoni mwa timu ambazo zitashiriki mashindano hayo ya kufuzu AFCON ambapo kikosi hicho kipo chini ya Kocha Mkuu, Kim Poulsen.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa