Mwamuzi wa kati wa mchezo kati ya Young Africans dhidi ya Azam, na mchezo kati ya Tz Prisons dhidi ya Simba, Ahmed Arajiga, na mwamuzi msaidizi namba moja wa mchezo( Young Africans dhidi ya Simba)  Frank Komba kutoka Dar es salaam wamepelekwa kamati ya maadili TFF.

 

Arajiga na Komba Wapelekwa Kamati ya Maadili

Maamuzi hayo ya kupelekwa kamati ya maadili yamekuja baada ya waamuzi hao kuonekana  kushindwa kumudu michezo hiyo ambapo mchezo ya Azam FC uliisha kwa sare ya mbili kwa mbili, huku mchezo wa Simba dhidi ya Prison, Simba akichukua alama 3.

Matukio hayo ya waamuzi yamekuwa ni sugu nchini kwetu ambapo waamuzi wamekuwa wakikosa umakini wakati wakichezesha mechi na kupelekea timu moja kati ya hizo mbili zinazocheza kuonewa na nyingine kunufaika.

 

Arajiga na Komba Wapelekwa Kamati ya Maadili

Ahmed Arajiga amechukua tuzo ya mwamuzi bora msimu uliopita huku Frank Komba pia akichukua tuzo ya mwamuzi bora msaidizi lakini, kwa upande wa Arajiga amekuwa na sintofahamu nyingi kutokana na kushindwa kumudu baadhi ya mechi hasa zikiwa timu kubwa zinacheza dhidi ya timu za daraja la kati au ndogo kabisa.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa