Kevin De Bruyne ndiye “mchezeshaji bora Duniani” kulingana na kocha mkuu wa Ubelgiji Roberto Martinez, ambapo kiungo huyo wa Manchester City alipochangia bao na kusaidia katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Wales.

 

Martinez: De Bruyne ni Mchezashaji Bora Duniani

De Bruyne ambae ndiye mchezaji bora wa ligi msimu uliopita wa ligi kuu ya Uingereza, pia alipiga shuti la kipindi cha kwanza lililogonga lango.

“Ni ujumbe kwa mashabiki wetu wote, usimchukulie kirahisi kumtaja Kevin De Bruyne akicheza,” Martinez aliwaambia wanahabari. “Kwangu mimi ndiye mchezeshaji bora zaidi katika soka la Dunia kwa wakati huu”.

“Njia yake ya kuona mchezo, njia yake ya kuona wakati, na nafasi na kisha utekelezaji mbele ya lango . Martinez  anasema kuwa alidhani kuwa uchezaji wa De Bruyne ulikuwa kama wa kimiujiza, lakini amekuwa akifanya hivyo, akiangalia mechi kadhaa hata ile dhidi ya Poland ambapo amekuwa akifanya hivyo mara kwa mara amekuwa akimtazama mara kwa mara, na wamekuwa na bahati sana ya kuwa na Kevin De Bruyne.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 ambaye ni mchezaji bora wa soka msimu uliopita alikuwa wa pili katika maisha yake ya soka, pia akipata heshima hiyo msimu wa 2019/20 na sasa anaongoza ligi kuu akiwa ametoa assist 6.

 

Martinez: De Bruyne ni Mchezashaji Bora Duniani

Hivi majuzi, De Bruyne ni mwanachama wa timu bora ya mwaka PFA mara nne na ameisadia City kutwaa mataji manne ya Ligi kuu. Pia alishinda kiungo bora wa ligi ya Mabingwa wa 2019/20. Halikadhalika Mbelgiji huyo alitajwa kuwa miongoni mwa walioteuliwa mwezi uliopita kuwania Ballon d’Or mwaka huu na msindi kutangazwa Oktoba, baada ya kushika nafasi ya nane mwaka 2021.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa