Eden Hazard ameapa kurejea kwenye kiwango chake bora mara tuu “hali yake tete” huko Real Madrid itakapotatuliwa.

 

Hazard Aapa Kurejea kwenye Ubora Wake

Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Ubelgiji alionyesha kiwango cha hali ya juu wakati wa dakika 65 alizocheza uwanjani kwenye ushindi wa 2-1 wa ligi ya Mataifa dhidi ya Wales siku ya Alhamisi .

Huu ndio ulikuwa mchezo mrefu zaidi ambao Hazard amecheza katika mechi moja msimu huu, akiwa amewekewa vikwazo vya kuanza mara moja katika mechi tisa za Madrid, kila moja ikiisha kwa ushindi.

Nafasi ya Hazard katika kikosi cha Ubelgiji imetiliwa shaka kabla ya Kombe la Dunia, na mshambuliaji huyo wa zamani wa Chelsea alikiri kwamba anahitaji kucheza mara kwa mara zaidi. “Nilikuwa nina furaha kuanza mechi nyingine” Aliiambia RTL.”Uliona hilo nadhani. Nina furaha ninapocheza na ilikuwa na ilikuwa nzuri kuchezea wafuasi hapa tena.

Hazard alisema kuwa anajua anachoweza kufanya na anataka kujiweka sawa kuelekea Kombe la Dunia tutaona kila ambacho kocha Roberto Martinez ataamua ila nina furaha sana ninapocheza.

 

Hazard Aapa Kurejea kwenye Ubora Wake

Mitchy Batshuay na Kevin De Bruyne waliweza kuchangia mabao mawili kwenye mchezo wa jana ambapo waliibuka na ushindi wa 2-1. Kikosi cha Martinez kimesalia na pointi tatu dhidi ya vinara wa kundi A4 Uholanzi kabla ya kusafiri kwenda Amsterdam Jumapili kwa mchezo wao wa mwisho.

“Tutajaribu kucheza mchezo mzuri huko na kujitayarisha kwa Kombe la Dunia” Hazard alisema.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa