Mchezaji wa klabu ya Yanga Bernard Morrison amefungiwa mechi tatu na kutozwa faini ya shilingi Milioni moja (100,0000) na kamati ya uendeshaji na usimamizi wa Ligi ya bodi ya ligi kuu Tanzania (TPLB).

 

Morrison Afungiwa na TPLB

Adhabu hiyo imekuja baada ya Morrison kumkanyaga kwa makusudi mchezaji wa klabu ya Azam FC Lusajo Mwaikenda katika mchezo wa Ligi kuu ambao Yanga waliwakaribisha Azam FC katika uwanja wa Benjamini Mkapa.

Haikuishia hapo, kamati hiyo pia imemfungia Bernard mechi tatu zijazo ambapo mechi ya kwanza ni ile ambayo itapigwa Oktoba 3 dhidi ya Ruvu Shooting, mechi nyingine ni tarehe 13 watakayoumana na Namungo kutoka Lindi na mechi ya mwisho ambayo ataikosa ni Dabi itakayowakutanisha wao na wapinzani wao wakuu, watani wao wa jadi Simba, ambapo itakuwa ni Oktoba 23.

 

Morrison Afungiwa na TPLB

Mchezaji huyo ambaye amecheza vilabu vyote viwili Simba pamoja na Yanga na Hatimae kurudi Yanga amekuwa haishiwi vituko vya hapa na pale, amekuwa akikumbwa na adhabu kila msimu kutokana na kukosa nidhamu kuanzia uwanjani hadi nje ya uwanja.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa