Klabu ya Liverpool FC inalazimika kufanya mabadiliko ya haraka kwenye mipango yake ya usajili wa majira ya joto kufuatia taarifa za majeruhi makubwa ya mshambuliaji Hugo Ekitike.
Nyota huyo wa Ufaransa anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa miezi kadhaa baada ya kupata jeraha la kisigino cha mguu kwenye mchezo dhidi ya Paris Saint-Germain.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kwa mujibu wa vyanzo vya ndani, hali hiyo inalazimisha klabu hiyo ya Merseyside kuharakisha mikakati yake ya kuimarisha safu ya ushambuliaji, hasa wakati huu ambapo pia kuna uwezekano wa kuondoka kwa Mohamed Salah mwishoni mwa msimu huu. Aidha, mustakabali wa kocha Arne Slot bado haujathibitishwa huku nafasi ya kushiriki UEFA Champions League msimu ujao ikiwa haijawa ya uhakika.
“Jeraha la Ekitike pamoja na uwezekano wa kuondoka kwa Salah, vinaacha pengo kubwa kwenye safu ya ushambuliaji kwa upande wa Liverpool,” chanzo kimoja kilieleza. “Klabu inalazimika kutafuta suluhisho la haraka ili kurejesha makali yao mbele ya lango.”
Taarifa zinaeleza kuwa Liverpool sasa inatazama njia mbili kuu sokoni; moja ikiwa ni kutafuta mbadala wa moja kwa moja wa Salah, na nyingine ni kusajili mshambuliaji mwenye uwezo wa kucheza nafasi mbalimbali. Miongoni mwa majina yanayotajwa ni Francisco Conceicao wa Juventus na Yan Diomande wa RB Leipzig.
Hata hivyo, kutokana na hatari ya kufanya makosa kwenye usajili, Liverpool inaelekea zaidi kwa wachezaji waliothibitisha ubora wao ndani ya Ligi Kuu England. Anthony Gordon wa Newcastle United ni miongoni mwa wanaotazamwa kwa karibu, huku pia Jarrod Bowen wa West Ham United akitajwa kuwa chaguo jingine muhimu. “Mipango ya usajili inaendelea kwa kasi kubwa,” chanzo kingine kiliongeza. “Lengo ni kuhakikisha majina ya mwisho yanaamuliwa ifikapo Mei, ili Liverpool iwe tayari kuingia sokoni mara tu dirisha litakapofunguliwa.”

