Klabu ya Azam FC imethibitisha kuwa mchezo wake dhidi ya Yanga SC utachezwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, badala ya Azam Complex, Jumapili, Machi 15, 2026.

Afisa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Thabit Zakaria ‘Zaka Zakazi’, amesema uamuzi huo umechukuliwa baada ya wamiliki wa Uwanja wa Benjamin Mkapa kuruhusu matumizi yake, huku ukarabati wa Uwanja wa Azam Complex bado haujaanza.
“Kabla ya msimu kuanza, tulichagua kutumia Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa mechi zetu mbili za nyumbani dhidi ya Yanga na Simba. Tulipokuwa tukipanga mechi dhidi ya Yanga, tukaangalia uwezekano wa kutumia Uwanja wa Azam Complex, lakini wamiliki wa Benjamin Mkapa walisema kwamba ukarabati haujaanza, hivyo tunaweza kuutumia,” amesema Zaka.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Zaka aliongeza kuwa uwanja huo umewapa Azam FC faida kutokana na rekodi yao ya kushinda Yanga mara nyingi pale, na alihakikisha mashabiki kwamba hakuna hofu ya kukutana na Yanga katika mchezo huo. “Tunaamini tutapata matokeo mazuri,” Kumbuka mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu uliochezwa na Azam FC katika Uwanja wa Benjamin Mkapa ulikuwa wa mzunguko wa kwanza dhidi ya Simba SC.

