Nyota wa Chelsea FC, Pedro Neto, amemuomba msamaha kijana anayeokota mpira (Ball Boy) baada ya kumsukuma katika mchezo wa UEFA Champions League uliofanyika Parc des Princes, Ufaransa, jana usiku wakati Chelsea walipokubali kichapo cha mabao 5-2 kutoka PSG.

Neto alisema kuwa kitendo hicho kilitokea kwa hasira ya kucheza baada ya kupoteza mchezo na alijutia matendo yake. “Nimemwomba msamaha kwa kumpa na jezi yangu, ni hasira tu ya kufungwa iliyosababisha nifanye tukio lile ambalo sikutarajia. Najutia kosa langu,”
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Tukio hilo limevutia hisia mchanganyiko katika vyombo vya habari na mashabiki wa soka, huku wengi wakihofia athari zinazoweza kumtokea Neto kutokana na kitendo hicho. Hali hii pia inatia shaka kuhusu uwezekano wa UEFA kumchukulia hatua za kinidhamu kwa Neto, kwani mashirika ya soka barani Ulaya huchukua hatua kali dhidi ya kitendo chochote kinachohusiana na kadhia za Ball Boy.
Kwa sasa, inatarajiwa kuwa UEFA itatoa uamuzi wake katika siku za karibuni, jambo ambalo linaweza kuwa adhabu au onyo kwa nyota huyo wa Chelsea kutokana na tukio hilo.

