Pioli: Ibrahimovic Anabaki Milan Kutokana na Umuhimu Wake.

Kocha mkuu wa AC Milan Stephano Pioli amesema kuwa Zlatan Ibrahimovic ataendelea kusalia klabuni hapo kwasababu ya matokeo chanya anayoyatoa klabuni hapo wakati wakisubira apone majeraha yake ya goti aliyoyapata.

 

Pioli: Ibrahimovic Anabaki Milan Kutokana na Umuhimu Wake.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 41, ambaye amefunga mabao 33 katika mechi 60 za ligi katika kipindi chake cha pili akiwa na Rossoneri, alifanyiwa upasuaji mwezi Mei. Huku maisha ya Ibrahimovic yakionekana kuwa hatarini wakati huo, lakini nyota hyo wa Sweden amesema kuwa; “Nikiona mchezaji mwenye nguvu kuliko mimi, nitaacha ,lakini bado sijamuona.”

Taarifa zinasema kuwa mshambuliaji huyo hatarajiwi kuchezeshwa na Milan hadi 2023 huku Pioli akisema kuwa mshambuliaji huyo ni mzuri. Akizungumza kabla ya mechi ya leo dhidi ya Monza, kocha huyo amesema kuwa Zlatan katika kila kitu anachosema na kukifanya kamwe si kitu kidogo na ana akili sana.

Mshambuaji huyo kupona itachukua muda mrefu kidogo, na pia itachukua muda kumuona tena uwanjani huku mashabiki wakimsubiria kwa hamu arejee.

AC Milan kwenye Serie A, wameshinda mechi sabakati ya 10 za kwanza msimu huu wakiwa kama mabingwa watetezi kwa mara ya kwanza tangu 1992-93, lakini mpaka sasa wapo nyuma kwa pointi tatu dhidi ya kinara wa Ligi hiyo Napoli.

Pioli: Ibrahimovic Anabaki Milan Kutokana na Umuhimu Wake.

Hata hivyo, Pioli anaamini kuwa timu yake inastahili kushinda pointi nyingi zaidi kuliko ilizopata huku akisema kuwa kwa maoni yake timu yake ilistahili kukusanya pointi nyingi zaidi ya hizo, walipoteza dhidi ya Napoli na baade wakawa na hali mbaya ambapo wanahitaji kujiimarisha.

Amesisitiza kuwa kiwango chao lazima kiwe cha juu kila wakati, pia akatoa taarifa kuhusu hali ya Mike Maignan kufuatia ripoti zinazodai kuwa golikipa huyo wa Ufaransa anaweza kukosa Kombe la Dunia baada ya kupata jeraha la mguu.

Pioli: Ibrahimovic Anabaki Milan Kutokana na Umuhimu Wake.

Ingawa kukosekana kwa Maignan kungeifanya Ufaransa kukosa ushindani kati yake na  Hugo Lloris, ripoti za vyombo vya habari vya Ufaransa zimedai kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 bado anaweza kupona kwa wakati na kusafiri kwenda Qatar, na maneno ya Pioli yanasemekana kuwa yanahusu klabu yake pekee.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.